Psalms 84

Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.

1 aEe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
makao yako yapendeza kama nini!
2 bNafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua za Bwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai.

3 cHata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima.

5 dHeri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
6 eWanapopita katika Bonde la Baka,
Yaani Bonde la Vilio.

hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.
Au: baraka.

7 hHuendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.

8 iEe Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu;
nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
9 jEe Mungu, uitazame ngao yetu,
mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.

10 kSiku moja katika nyua zako ni bora
kuliko siku elfu mahali pengine;
afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu
kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
11 lKwa kuwa Bwana ni jua na ngao,
Bwana hutoa wema na heshima;
hakuna kitu chema anachowanyima
wale ambao hawana hatia.

12 mEe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.
Copyright information for SwhNEN